Uchaguzi wa Guinea: Rais Alpha Conde Awania Muhula Wa Tatu

Raia wa Guinea wapatao milioni 5.4 watashiriki kwenye zoezi la kupiga kura leo hii Jumapili 18.10.2020 ambapo rais Alpha Conde anawania muhula wa tatu wa urais. Hatua ya Conde ya kuwania muhula mwingine wa urais imesababisha ghasia na chuki miongoni mwa watu wa Guinea. 

Rais Alpha Conde mwenye umri wa miaka 82 anagombea muhula wa tatu baada ya katiba kubadilishwa. Kwa mujibu wa shirika la haki za binadamu la Amnesty International, takribani watu 50, wengi wao wakiwa wapinzani, waliuawa mnamo mwaka uliopita kwenye maandamano ya kupinga kubadilishwa kwa katiba nchini Guinea. Amnesty International imesema vurugu zilitokea kwa mfululizo katika kipindi cha wiki za hivi karibuni wakati wa kampeni.

Conde, aliwaambia wafuasi wake katika mkutano wake wa mwisho wa kampeni siku ya Ijumaa uliofanyika kwenye uwanja wa mpira katika mji mkuu, Conakry kwamba mageuzi ya katiba yaliyoidhinishwa katika kura ya maoni mnamo mwezi Machi yalikuwa ya haki na ya kidemokrasia, amesema anahitaji muda zaidi madarakani kuweza kumaliza mipango mikubwa katika sekta ya madini makubwa na miradi ya kuboresha miundombinu.


EmoticonEmoticon