UEFA
wametangaza kuwa wataruhusu mashabiki kuingia uwanjani katika mechi za
Champions League na timu ya taifa kwa asilimia 30 ya uwezo wa uwanja kuchukua
mashabiki.
Uamuzi huo utatekelezwa
endapo sheria za taifa husika hazitakuwa zinazuia, kingine katika michezo hiyo
mashabiki wa timu mgeni hawatoruhusiwa kuingia viwanjani kama tahadhari ya
Corona.
Hii ni ishara njema na inakuja ikiwa ni miezi takribani saba toka michezo isimame na mashabiki kutoruhusiwa kuingia viwanjani kutokana na kuingia kwa virusi vya Corona katika mataifa ya Ulaya mwezi March 2020.
EmoticonEmoticon