Uganda Yapiga Hatua Katika Kuanza Kuchimba Mafuta

 

Kampuni ya kuchimba mafuta ya Tullow imepata ruhusa kutoka kwa serikali ya Uganda, kuuza mgao wake wa machimbo ya mafuta katika eneo la ziwa Albert kwa kampuni ya Ufaransa ya Total.

Hatua hiyo inatarajia kutoa fursa ya kuanza kwa hatua ya mwisho ya uwekezaji katika kuchimba na kusafirisha mafuta ya Uganda kwa soko la kimataifa, ikiwemo ujenzi wa bomba la kusafirisha mafuta hao kutoka Hoima Uganda hadi Tanga, Tanzania.

Katika taarifa kwa vyombo vya habari, kampuni ya Tullow imesema kwamba serikali ya Uganda na mamlaka ya kukusanya ushuru Uganda - URA, zimefikia makubaliano kuhusu namna ya kulipa ushuru kutokakana na kuuza kwa vifaa vyake kwa kampuni ya Total.

“Waziri wa nishati na maendeleo ya madini wa Uganda ameidhinisha hatua ya kupeana vifaa na mali za Tullow kwa kampuni ya Total pamoja na idhini ya utendaji kazi katika machimbo namba 2,” inesema taarifa ya Tullow, ikiendelea kusema kwamba “kwa sababu masharti yote ya serikali yametimizwa, Tullow inatarajia kumaliza shughuli zake katika muda wa siku chache zijazo na kupokeza idhini ya kufanya kazi kwa Total.”

Kampuni ya Tullow itapokea dola milioni 500 katika hatua ya kwanza na dola milioni 75 maamuzi ya uwekezaji ya mwisho yatakapochukuliwa kuhusu mradi huo wa kuchimba mafuta.

Kampuni ya Tullow pia ina haki ya kupokea sehemu ya pesa zitakazopatikana katika awamu ya kwanza ya uchimbaji mafuta hayo.

Tangu mwaka 2016, Uganda imekuwa ikikumabana na changamoto kadhaa za kisheria, kuhusiana na uchimbaji mafuta yake yanayotarajiwa kuielea dola bilioni 3.5.


EmoticonEmoticon