Uingereza Na Kenya Kukusanya Dola Bilioni Tano Kufadhili Elimu Baada Ya Covid-19

 

Waziri Mkuu wa Uingereza na Boris Johnson na Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta wanatarajiwa kuzindua mpango utakaosaidia kukusanya dola bilioni tano sawa na (£3.8bn) kwa ajili ya kuwasomesha watoto kutoka jamii masikini duniani

Idadi ya wanafunzi walioacha shule imeongezeka zaidi wakati wa janga la Covid-19.

Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, Sayansi na utamaduni (Unesco) linakadiria kuwa hadi wanafunzi bilioni 1.3 duniani billioni wameacha shule huku wataalamu wakionya kuwa baadhi yao huenda wasirudi kutokana na hali ya kiuchumi ya nchi zao.

Viongozi hao wawili pia watatangaza mpango wa kuandaa kwa pamoja kongamano kuu la elimunchini Uingereza katikati yam waka ujao kutafuta ungwaja mkono.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson na Rais Uhuru Kenyatta watawashawishi viongozi kuhakikisha wanaenda shulewa kuwekeza zaidi katika mpango huo unaofahamika kama Global Partnership for Education.


EmoticonEmoticon