Ujerumani Yaamua Kuanzisha Hatua Kali Kudhibiti Corona

 

Kufuatia kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya virusi vya corona nchini Ujerumani, serikali kuu ya nchi hiyo pamoja na serikali za majimbo zimekubaliana juu ya hatua kali za kudhibiti maisha ya kawaida kuanzia mwezi ujao wa Novemba. 

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, alisema jana baada ya mkutano wa mtandaoni na wakuu wa serikali za majimbo kwamba ilikuwa "siku ngumu" kwa sababu kila moja wao alijua hali ngumu watakayopitia watu kutokana na maamuzi hayo. 

Kwa mujibu wa kansela huyo, kuna masharti makali, hasa ktika sekta ya starehe. Juu ya hayo, mawasiliano binafsi pia yamedhibitiwa vikali. Kwa upande mwingine, maisha ya kiuchumi yataendelea kama kawaida na shule pamoja na vituo vya uangalizi watoto vitaendelea kuwa wazi.


EmoticonEmoticon