Ujumbe Wa Serikali Ya UAE Waenda Israel

 

Ujumbe wa kwanza rasmi wa Umoja wa Falme za Kiarabu umeondoka leo nchini humo kwenda Israel wakati nchi hizo mbili zinaangalia kupanua ushirikiano wao baada ya kurejesha uhusiano wao mwezi uliopita chini ya makubaliano yaliyosimamiwa na Marekani, yaliyofikiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na hofu ya nchi hizo kuhusu Iran. 

Ndege ya shirika la ndege la Etihad iliyowabeba maafisa wa serikali pamoja na maafisa wa Marekani wanaoongozana nao, iliondoka katika mji mkuu wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Abu Dhabi, ikielekea katika uwanja wa ndege wa Ben-Gurion.

Maafisa wa Israel hata hivyo wamesema ziara hiyo itaishia uwanja wa ndege kutokana na wasiwasi wa maambukizi ya virusi vya corona. Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain mwezi Septemba zimekuwa nchi za kwanza za Kiarabu katika zaidi ya miaka 25 kutia saini makubaliano ya kurejesha uhusiano na Israel.


EmoticonEmoticon