Viongozi 40 Wa Belarus Kuwekewa Vikwazo Na Umoja Wa Ulaya

 

Viongozi wa mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya wamekubaliana kuwawekea vikwazo maafisa 40 wa Belarus kwa kughusi uchaguzi pamoja na ukandamizaji dhidi ya waandamanaji isipokuwa Rais wa nchi hiyo Alexander Lukashenko. 

Viongozi wa Umoja wa Ulaya mapema leo wamekubaliana kuwawekea vikwazo maafisa wa Belarus, na kumaliza mkwamo na Cyprus iliyokuwa ikizuia kutekelezwa kwa hatua hiyo baada ya umoja huo kukubali kuitumia onyo kali Uturuki.

Vikwazo hivyo vinawalenga maafisa 40 wa Belarus, kwa kughushi uchaguzi pamoja na kuwakandamiza waandamanaji walioingia mitaani kupinga matokeo ya uchaguzi wa Agosti 9 uliompa ushindi Rais wa Belarus Alexander Lukashenko.


EmoticonEmoticon