Watu kadhaa
walioandamana dhidi ya polisi wakatili wameripotiwa kupigwa risasi na kufa na
huku wengine wakiwa wamejeruhiwamjini Lagos, Nigeria.
Walioshuhudia
tukio hilo wameiambia BBC kuwa wameona miili ipatayo 20 ilikuwa imetapakaa na
wengine 50 wamejeruhiwa baada ya wanajeshi kufyatua risasi.
Shirika
la kimataifa la Amnesty limesema limepata habari za kuaminika kuhusiana na vifo
hivyo.
Maafisa wameahidi kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo. Amri ya kutotoka nje ndani ya saa 24 imewekwa mjini Lagos na miji mingine.
Waandamanaji
sasa wamezunguka vituo vya polisi , kikosi maalum cha Sars, kimekuwa
kikiendelea kwa muda wa wiki mbili .
Kutokana
na mapigano ya risasi yanayoendelea , aliyekuwa waziri wa mambo ya nje Marekani
bi. Hillary Clinton amemtaka rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kuacha kuwaua
vijana asitishe maandamano ya Sars.
#EndSARS
".
Mcheza mpira Nigeria Odion Jude Ighalo, ambaye anaichezea Manchester United, ameishutumu serikali ya Nigeria kwa kuua wananchi wake. Alisema hayo kupitia ukurasa wa tweeter kwa kuweka video.
EmoticonEmoticon