Wabunge Wa Malawi Wakataa Msaada Wa Kondomu

Wabunge nchini Malawi wamekataa kupokea msaada wa mipira ya kondomu zaidi ya 200,000 waliyopewa na shirika moja la kutoa misaada.

Mipira hiyo ilikuwa iwekwe katika vyoo vya majengo ya bunge.

Kiongozi wa wengi bungeni, Richard Chimwendo, amesema wabunge hawahitaji msaada huo kwasababu wana uwezo wa kumudu bei ya kondomu.

Msaada huo ulipewa mwenyekiti wa kamati ya, Maggie Chinsinga.

Bw. Chimwendo alisema ripoti iliyochapishwa na gazeti moja nchini humo kwamba msaada huo umewadhalilisha wabunge.

Ripoti hiyo ilimnukuu Bi Chinsinga akisema kuwa bunge hutumia karibu mipira 10,000 ya kondomu kila mwezi na kwamba wakati mwingine "zinaisha", iliandika gazeti la Nation nchini Malawi.

Naibu wa Spika, Madaliotso Kazombo, amekanusha madai haya na kutaka gazeti hilo kuomba radhi.


EmoticonEmoticon