Ukusanyaji wa
maoni ulioendeshwa na shirika la habari la Reuters kwa ushirikiano na taasisi
ya Ipsos umeonyesha kuwa zaidi ya wafuasi wanne kati ya kumi wa rais Donald
Trump na mpinzani wake Joe Biden, wamesema hawatokubali matokeo ya uchaguzi wa
Novemba iwapo mgombea wanayemuunga mkono atashindwa.
Utafiti huo ambao
uliendeshwa kati ya tarehe 13 na tarehe 20 Oktoba unaonyesha asilimia 43 ya
wafuasi wa Biden hawatokubali ushindi wa Trump, na asilimia 41 ya wale
wanaotaka Trump achaguliwe kwa muhula wa pili hawatokubali ushindi wa Biden.
Asilimia 22 ya wafuasi wa
Biden na asilimia 16 ya wafuasi wa Trump wamesema wako tayari kufanya
maandamano hata kujihusisha na vitendo vya vurugu iwapo mgombea wanayemuunga
mkono atashindwa.
Maafisa wanaosimamia uchaguzi wanakabiliwa na changamoto nyingi mwaka huu na walielezea wasiwasi wao kuhusu Imani ya umma juu ya matokeo ya uchaguzi.
EmoticonEmoticon