Wafungwa 900 Watoroka Katika Uvunjaji Gereza Congo Mashariki

 

Wapiganaji wenye silaha wamewaachilia huru wafungwa wasiopungua 900 kutoka jela mjini Beni, mashariki mwa Congo, katika shambulio la kupanga mapema Jumanne, ambalo meya wa mji huo amelilaumu kwa waasi wa ADF. 

Zaidi ya wafungwa 900 wametoroka kutoka gereza la mji wa mashariki mwa Congo la Beni Jumanne, amesema meya, wakiwemo wanachama cha kundi la waasi wa Kiislamu la ADF.

Modesta Bakwanamaha alisema waasi kutoka kundi la Allied Democratic Forces, ADF, na makundi mengine ya waasi walikuwa miongoni mwa waliotoroshwa gerezani na washambuliaji waliotumia vifaa vya kuchomelea.

Ni wafungwa 100 tu kati ya zaidi ya 1,000 walibakia kufuatia shambulio dhidi ya gereza kuu la Kangbayi na kambi ya kijeshi iliyolilinda gereza hilo, alisema Meya Bakwanamaha.

"Kwa bahati mbaya, washambuliaji waliokuja katika idadi kubwa, walifanikiwa kuvunja mlango kwa kutumia kifaa cha umeme," Bakwanamaha aliliambia shirika habari la Reauters kwa njia ya simu. "Tunaamini ni ADF ndiyo walifanya uhalifu huu.


EmoticonEmoticon