Wapiga mbizi
wa jeshi la Poland wameanza operesheni ya hatari ya kunasua bomu kubwa la
Uingereza lililotumika kwenye vita vya pili vya dunia lililo chini ya bahari.
Karibu
wakazi 750 wameondolewa kutoka kwenye eneo hilo karibu na mji wa bandari wa
Swinoujscie, na operesheni hiyo inatarajiwa kuchukua siku 5.
Bomu
liitwalo Tallboy, au bomu la ''tetemeko la ardhi'' lina urefu wa mita 6 na
uzito wa tani 5.4.
Bomu
hilo lilidondoshwa wakati wa uvamizi mwaka 1945 ambapo tukio hilo lilizamisha
meli ya Ujerumani ya Lützow.
Bomu
hilo liko chini umbali wa mita 12 na kinachoonekana juu kikichungulia ni sehemu
ya pua ya kifaa hicho.
Kazi iliyopo
sasa ni kuhakikisha bomu hilo linaondolewa kwa kutumia combo maalumu kutoka
mbali, na wapiga mbizi tayari wameliandaa eneo hilo kwa siku kadhaa.
Bomu
hilo liligundulika wakati wa kufanya usafi wa bahari mwaka jana.
Poland
haijawahi kunasua bomu kubwa kama hilo chini ya maji hapo kabla. The Tallboy ni
bomu linalosababisha mtetemeko ,linalopenya chini, lililoundwa kwa ajili ya
kuangushwa karibu na eneo linalolengwa na kufanya uharibifu kwa kulipuka na
kusababisha tetemeko na mshtuko mkubwa.
Majeshi ya anga ya Uingereza yaliangusha mabomu ya aina hiyo mwaka 1944-45 kwa kutumia 'Lancaster bombers' na maeneo ya kurushia roketi ya jeshi la Ujerumani Nazi - V yalikua miongoni mwa maeneo yaliyokuwa yakilengwa.
EmoticonEmoticon