Wanamgambo 275 wa kundi la
Taliban wameripotiwa kuacha silaha na kujisalimisha kwa serikali katika mikoa
ya Sar-i Pul na Balkh kaskazini mwa Afghanistan.
Naibu
Msemaji wa Wizara ya Ulinzi Fawad Aman alitoa maelezo na kuelezea kwamba
wanamgambo 150 wa kundi la Taliban walijisalimisha serikalini wakiwa na silaha
zao mjini Balhab mkoani Sar-i Pul.
Aman
aliongezea kusema kuwa miongoni mwa wanamgambo hao, kulikuwa na makamanda 15 wa
kundi la Taliban.
Kwingineko
katika mji wa Charkent mkoani Belh, wanamgambo 125 walijisalimisha serikalini
na kuahidi kwamba hawatojihusisha tena na Taliban wala kupigana.
Kundi la
Taliban halijatoa maelezo yoyote kuhusiana na tukio hilo.
Kwa miaka mingi kundi la Taliban na wajumbe wa serikali ya Afghanistan wamekuwa wakiendesha mchakato wa kusitisha mapigano katika mji mkuu wa Doha nchini Qatar. Kitendo cha wanamgambo wa Taliban kujisalimisha makundi kwa makundi hasa kwa kipindi hiki kimekuwa cha kushangaza.
EmoticonEmoticon