Wanasayansi
wanaonya kuwa ziwa la lava linajaa kwa kiwango cha kutishajuu katika Mlima wa
volcano wa Nyiragongo uliopo juu ya mji wa Goma Mashariki mwa Jamuhuri ya
kidemokrasi ya Kongo.
Mwezi Januari 2002, lava iliyomwagika
ilimwagika kutoka Mlima Nyiragongo kwa kasi hadi katika mji wa Goma na
kusababisha vifo vya watu 250 na kuharibu 20% ya mji wa Goma.
Kikundi cha wanasayansi wanaochunguza
matukio ya milima, wameonya kuwa “mwamba unaoyeyuka unaweza kulipuka tena
kupitia kuta za ziwa la volkano”, imesema taarifa yajarida la kisayansi.
“ Sasa, hali inaonyesha dalili za
mkasa mwingine” Dario Tedesco, mtaalamu wa volcano na milima aliliambia jarida
la masuala ya kisayansi.
Tathmini yao
inaonesha kuwa hatari kubwa zaidi yam lima huo itatokea katika kipindi cha
miaka 4, ingawa wanaamini tetemeko la ardhi linaweza kusababisha mlipuko huo
mapema.
“Hii ni volkano hatari zaidi duniani!” Profesa Tedesco aliongeza. Watu wapatao milioni moja wanaishi katika mji wa Goma.
EmoticonEmoticon