Polisi
nchini Kenya wamethibitisha kwamba watu wawili walifariki katika makabiliano ya
siku ya Jumapili kati ya wafuasi wa Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William
Ruto.
Bw.
Ruto, ambaye alikuwa anahudhuria ibada ya kanisa katika eneo la Murang'a, ngome
ya rais Kenyatta iliopo eneo la kati Kenya, alilaani tukio hilo lililowalazimu
polise kurusha vitoa machozi ndani ya kanisa kuwatawanya vijana waliokuwa
wakishambuliana kwa mawe , kuchoma magurudumu ya magari na kufunga barabara kuu
na kusababisha msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo yenye shughuli
nyingi.
Rais Kenyatta - ambaye yuko nchini Ufaransa kwa ziara ya kikazi - na Bw. Ruto wametofautiana vikali katika hatua ambayo imewafanya maafisa wa chama tawala - Jubilee- kupendekeza naibu wa rais kuondolewa kama naibu kiongozi wa chama hicho kilichobuniwa mwaka 2012.
EmoticonEmoticon