Rais wa
Nigeria Muhammad Buhari amesema watu 69 wameuawa kwenye maandamano dhidi ya
ukatili wa polisi, maandamano yanayofanyika nchini humo.
Waliouawa
ni raia, maafisa wa polisi na wanajeshi, alieleza.
Shirika
la Amnesty International lilisema mwanzoni mwa wiki hii kuwa takribani watu 56
wamepoteza maisha tangu yalipoanza maandamano, ikiwemo waandamanaji 12
waliouawa jijini Lagos siku ya Jumanne.
Kundi
ambalo limekuwa mbele katika kuratibu maandamano sasa limewataka watu kubaki
majumbani mwao.
Umoja wa
wanaharakati wa wanawake pia umewataka watu kufuata masharti ya muda wa kuwepo
majumbani yatakayowekwa kwenye majimbo yao.
Mitaa ya
mji mkubwa wa Nigeria, Lagos yalikoanzaia maandamano hayo, imekuwa kimya lakini
hali ya hofu imeendelea kuwepo.
Maandamano yalianza tarehe 7 mwezi Oktoba huku vijana wakidai kuvunjwa kwa kikosi cha polisi cha SARS.
EmoticonEmoticon