Waziri wa
fedha wa Marekani, Steven Mnuchin, na Spika wa Baraza la Wawakilishi Nancy
Pelosi, walikutana Jumatano, ili kufikia muafaka juu ya msaada wa fedha kwa
raia wa Marekani.
Fedha hizo ni kwa ajili ya
kusaidia walioathiriwa na janga la virusi vya Corona, kabla ya bunge la
Marekani kusitisha vikao vyake na kwenda kwenye kampeni za uchaguzi wa Novemba
3.
Wawili hao walikutana
kujadili kwa kina yaliomo ndani ya muswada wa sheria ambao utatoa pesa zaidi
kwa familia za Wamarekani, na Wafanyabiashara.
Fedha zitalenga mamillioni
ya Wamarekani waliopoteza ajira, kutoa msaada wa fedha kwa majimbo na serekali
za wilaya, pamoja na kulinda biashara zisifilisike.
Tofauti ilioonekana kwenye
majadiliano hayo ni kuhusu kiwango cha msaada wenyewe.
Baraza la wawakilishi
linalodhibitiwa na Wademocrats linajiaanda kupitisha msaada wa dola trillioni
2.2, ambao unapingwa na Warepublican.
Waziri Mnuchin ambaye
anamuwakilisha rais Trump, ameiambia televijeni ya CNBC kwamba pendekezo la
White House ni dola trillioni 1.5
Spika Pelosi ameiambia televijeni ya MSNBC kwamba ana matumaini ya kupatikana mkataba licha ya kuwa Wademocrats na Warepublican wanatofautiana kuhusu kiwango cha pesa ambacho kinapaswa kutolewa.
EmoticonEmoticon