Angela Merkel Atoa Wito Wa Mshikamano Wa Kimataifa Dhidi Ya Corona

Viongozi wa nchi zenye nguvu kiuchumi duniani wanafanya mkutano kwa njia ya video kujadili namna ya kupambana na corona na kuufufua uchumi wa ulimwengu.

Viongozi wa nchi zenye nguvu kiuchumi duniani wanafanya mkutano kwa njia ya video kujadili namna ya kupambana na corona na kuufufua uchumi wa ulimwengu. 

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amewahimiza viongozi wa nchi za G20 kuendelea kushirikiana katika vita dhidi ya virusi vya corona, akiuambia mkutano wa kilele unaofanyika kwa njia ya video kuwa mengi yanastahili kufanywa ili kulidhibiti janga hilo.

Merkel aliyasema hayo wakati wa mkutano ulioandaliwa na Saudi Arabia na wakuu wa nchi na serikali kutoka madola yenye nguvu za kiuchumi duniani. 

"Tukisimama pamoja duniani, tunaweza kudhibiti na kukishinda kirusi hiki na madhara yake. Kwa hiyo juhudi zaidi inafaa.” Alisema katika ujumbe wa video.

Merkel amesema hii ni changamoto ya ulimwengu ambayo inaweza tu kukabiliwa kwa kushirikiana na mashirika ya kimataifa kama vile Shirika la Afya Ulimwenguni – WHO, Umoja wa Mataifa na G20, akiongeza kuwa viongozi wanahitaji kutoa fedha zaidi kuyasaidia mataifa maskini kupata chanjo.

Maneno yake yaliungwa mkono na Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye pia aliwahutubia viongozi.

"Tunakabiliwa na mgogoro wa kiafya unaotishia maisha ya mamilioni ya watu,” Alisema Macron. "Lakini hapawezi kuwa na jibu mwafaka kwa janga hilo kama sio la kimataifa, lililoratibiwa na linalotokana na mshikamano.”

Mkutano huo wa kilele unaandaliwa kwa njia ya video na wenyeji Saudi Arabia kutokana na janga la corona.


EmoticonEmoticon