Armenia, Azerbaijan, Urusi Zakubaliana Kumaliza Vita Vya Karabakh

 

Armenia na Azerbaijan zimetangaza mapema leo makubaliano ya kusitisha mapigano kuhusu mkoa wa Nagorno-Karabakh ulioko Azerbaijan chini ya muafaka uliotiwa saini na Urusi

Wanajeshi wa kulinda amani wa Urusi wamepelekwa mapema leo katika mkoa ulioharibiwa k Mpango huo, uliosainiwa na Armenia, Azerbaijan na Urusi, ulioanza kutekelezwa usiku wa manane jana umefuatia mgogoro uliowauwa maelfu ya watu, kusababisha wengi kupoteza makazi na kutishia kuitumbukiza kanda hiyo nzima katika vita.

Chini ya mkataba huo, Azerbaijan itayadhibiti maeneo yote iliyoyakamata, ukiwemo mji wa pili kwa ukubwa wa mkoa huo, Shusha, nao wanajeshi wa Kiarmenia wasalimishe udhibiti wa maeneo mengine kadhaa kati ya sasa na Desemba mosi.

wa vita wa Nagorno-Karabakh kama sehemu ya mpango wa kusitisha mapigano ambao Rais Vladmir Putin amesema utasafisha njia ya kupatikana suluhisho la kudumu la kisiasa kwa mgogoro wa eneo hilo.


EmoticonEmoticon