Askari Magereza Akiri Kufanya Mapenzi Na Mfungwa Wa Kosa La Mauaji

 

Mama wa watoto watatu ambaye pia ni askari magereza, amekiri kufanya mapenzi na mfungwa wa kosa la mauaji.

Mwanamke huyo Lauren McIntyre (32) jana alikutwa na hatia ya makosa manne ya utovu wa nidhamu kwenye ofisi ya Umma.

Mama huyo wa watoto watatu ikiwemo mapacha wawili wa miezi 11 na mmoja mwenye umri wa miaka 5, ameiambia mahakama kwamba ni kweli alikuwa na mahusiano na mfungwa huyo aitwaye Andrew Roberts kwenye gereza la Albany nchini Uingereza.

Alisema alianza mahusiano ikiwa ni kwenye mpango wa kiintelijensia kubaini ukweli wa makosa ya Andrew lakini alinogewa na kujikuta amezama kwenye penzi la mfungwa huyo mwenye makosa mawili ya mauaji.

Andrew alikutwa na hatia ya makosa hayo mwaka 2003 kwa kumnyonga binti wa miaka 8, alihukumiwa kifungo cha maisha.


EmoticonEmoticon