Biden Anaweza Kurudisha Ushirikiano Wa Kimataifa Na Uongozi?

 

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameapa kuondokana na sera ya nchi kujichukulia maamuzi. 

Lakini ili kuweza kurejesha uongozi wa Marekani atahitaji kurejesha Imani ya washirika waliotengwa na kuwawajibisha wapinzani. 

Biden ameapa kurejesha jukumu la uongozi wa Marekani duniani kwa kuibatilisha sera ya kujichukulia hatua kwa upande mmoja iliyowekwa na utawala wa Trump na kuangazia upya miungano ya muda mrefu ya kimataifa. 

Anasema serikali yake itaboresha diplomasia na kuongoza kwa kile alichokiita "nguvu ya mfano” na sio "mfano wa nguvu.”

Biden amerithi hali ambayo washirika wanahoji uadilifu wa Marekani, huku mahusiano kati ya Marekani na madola mengine ulimwenguni yakiwa mabaya.

Rais mteule ameapa kurekebisha uharibifu huo kadri inavyowezekana katika siku zake za kwanza 100 madarakani kwa kubatilisha amri kadhaa zilizosainiwa na Rais Donald Trump. 

Amri hizo zilisitisha makubaliano ya kimataifa na miungano ambayo rais alidai haikuwa ya haki kwa Marekani kutokana na sababu mbalimbali. 

Wakosoaji wanasema hatua hizo hazikuleta tija na kujitenga kwa Marekani kuliiruhusu China kuutanua uwepo wake kutokana na pengo la Marekani. 

Hizi hapa baadhi ya sera za kigeni ambazo rais huyo mteule ameapa kuzibatilisha mara moja:

1. Mkataba wa Nyuklia wa Iran

2. Makubaliano ya Tabia nchi ya Paris

3. Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)

4. Umoja wa Mataifa

5. WTO, NATO na Seneti


EmoticonEmoticon