Bobi Wine Aachiwa Kwa Dhamana

 

Baada ya kukamatwa na Polisi juzi kwenye mkutano wa kampeni kwa tuhuma za kukiuka kanuni za kujikinga na corona, Mgombea Urais wa kambi ya upinzani anaechuana na Museveni, Robert Kyagulanyi (Bobi Wine) ameachiwa kwa dhamana.

Wakati idadi ya waliofariki Uganda kutokana na fujo za uchaguzi ikifika 30 kwa mujibu wa dw huku zaidi ya 500 wakiwa wamekamatwa na Polisi, Waziri wa Afya amesema Serikali itagharamia matibabu ya Watu wote waliojeruhiwa kwenye maandamano ya kutaka Bobi Wine aachiwe huru.


EmoticonEmoticon