Bobi Wine Asema Museveni Anakabiliwa na Kizazi Chenye Hasira na Njaa

 

Mgombea urais wa upinzani nchini Uganda Robert Kyagulanyi, maarufu Bobi Wine, amesema Rais wa Yoweri Museveni anakabiliana na kizazi ambacho kitafanya kila iwezelo kupigania uhuru.

Alisema hayo katika hafla ya maombi iliyoandaliwa katika makao makuu ya chama chake kuwaomea watu waliouawa katika maandamano ya siku mbili yaliyokumba nchi, siku moja baada ya kuachiwa kutoka kizuizini.

Akimlenga moja kwa moja kiongozi wa nchi moja kwa moja Bobi Wine alisema Bwana Museveni anakabiliwa na kizazi ambacho kina njaa na hasira kwa wakati mmoja.

Hakuna kiwango chochote cha mabomu ya machozi au mateso ambacho kitawaogopesha, aliongeza.

Mgombea huyo wa urais amesema mashambulio yaliyofanywa dhidi ya raia wiki hii yameweka wazi udhalimu wa serikali ya sasa iliyo madarani.

Akiwahutubia wafuasi na maafisa wa chama, alisisitaiza kwamba damu ya raia wasiokuwa na hatia iliyomwagika wiki hii haitaenda bure, na kuongeza kuwa haki itatekelezwa.


EmoticonEmoticon