Boko Haramu Yauwa Wafanyakazi Wa Mashambani 43 Nigeria

 

Wapiganaji wa kundi la Boko Haram wamewauwa takribani wafanyakazi wa mashambani 43 na kujeruhi wengine sita katika mashamba ya mpunga karibu na mji wa kaskazini/mashariki mwa Maiduguri nchini Nigeria. 

Kundi la wanamgambo lenye kupinga itikadi kali limesema. Katika kijiji cha Kashobe washambuliaji waliwafunga wafanyakazi hao kwa kamba na kisha kuwachinja. 

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari amelaani shambulizi hilo kwa kusema "Nchi nzima imeumizwa na mauwaji hayo ya kipuuzi." 

Mmoja kati ya wapiganaji wapinga jihadi, Ibrahim Liman alisema waathirika walikuwa wafanyakazi kutoka jimbo la Sokoto, huko kaskazini/mashariki mwa Nigeria, umbali wa takribani kilometa 1,000, ambao walisafiri kwenda maeneo ya kaskazini/mashariki kwa ajili ya kutafuta kazi. 

Tangu 2009, zaidi ya watu 36,000 wameuwawa katika mzozo wenye kujikita katika itikadi kali, ambapo pia mzozo huo umesababisha takribani watu milioni mbili kuachwa bila ya makazi.


EmoticonEmoticon