Chanjo Ya Kampuni Ya AstraZeneca Dhidi Ya COVID-19 Yaonyesha Kufanya Kazi Vizuri Zaidi

 

Kampuni ya kutengeneza chanjo ya AstraZeneca imetangaza leo kuwa chanjo yao imethibitika kufanya kazi vizuri kwa asilimia 90, hatua inayowapa maafisa wa afya matumaini zaidi kwamba huenda ikapatikana chanjo hivi karibuni ambayo ni ya bei nafuu na rahisi kusambaza kuliko za washindani wengine. 

Matokeo hayo yametokana na tathmini ya awali ya majaribio yaliyofanywa nchini Uingereza na Brazil ya chanjo iliyoanzishwa na chuo kikuu cha Oxford kisha kutengenezwa na kampuni ya AstraZeneca.

Hakuna ripoti kuhusu yeyote miongoni mwa waliofanyiwa majaribio aliyelazwa hospitalini au kuwa na madhara mabaya. 

AstraZeneca ni kampuni ya tatu kutangaza matokeo ya awamu ya tatu ya majaribio ya chanjo zao za COVID-19, mnamo wakati ulimwengu unasubiri ufanisi utakaosaidia kulimaliza janga hilo ambalo limesababisha vifo vya takriban watu milioni 1.4 hadi sasa na pia kuathiri pakubwa chumi ulimwenguni.

Wiki iliyopita, kampuni za Pfizer na Moderna zilitangaza matokeo ya majaribio yao yaliyoonesha chanjo za okuwa na uwezo wa takriban asilimia 95 kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona.


EmoticonEmoticon