Diego Maradona Afanyiwa Mazinshi, Jeneza Lafunikwa Na Bendera

 

Mwanasoka Diego Maradona amefanyiwa mazishi katika sherehe ya kibinafsi katika mji wa Buenos Aires nchini Argentina siku moja baada ya kufariki dunia. Jamaa na marafiki wa karibu tu ndio waliohudhuria mazishi yake.

Lakini awali, kundi kubwa la watu lilijitokeza kutoa heshima zao za mwisho wengi wakiwa wanabubujikwa na machozi na kuonesha upendo. Maradona alifariki dunia kwasababu ya mshtuko wa moyo akiwa na umri wa miaka 60.

Kifo chake kimesababisha watu kumuombeleza kote duniani lakini hakuna walioomboleza kama raia wa nchi yake waliomchukulia kama shujaa wa taifa.

Jeneza la Maradona lilifunikwa bendera ya taifa na fulana ya mpira nambari 10 nafasi aliyocheza uwanjani - pia fulana hiyo ilikuwa inaoneshwa kwa umma katika makao ya rais.


EmoticonEmoticon