Waendesha
mashitaka nchini Argentina wanamchunguza daktari wa Diego Maradona kwa
uwezekano wa kuua kufuatia kifo cha nyota huyo wa soka kilichotokea siku nne
zilizopita .
Polisi mjini Buenos Aires wameisaka nyumba na kliniki ya
daktari huyo- Leopoldo Luque huku wakijaribu kubaini iwapo ulikuwepo uzembe
katika matibabu baada ya upasuaji aliofanyiwa Maradona.
Maradona ambaye alikuwa na umri wa miaka 60 alifariki dunia
kutoka na shinikizo la damu nyumbani kwake ambako alikuwa akiendelea kupona
baada ya kufanyiwa upasuaji.
Dokta Luque bado hajashitakiwa. Anakana kufanya kosa lolote.
Maradona alifanyiwa upasuaji kwenye mshipa wa ubongo kutokana
na kujganda kwa damu , uliofanikiwa mapema mwezi wa Novemba na amekuwa akipata
matibabu kutokana na uraibu wa pombe.
Binti yake alikuwa amesisitizia kupata taarifa zaidi kuhusu matibabu ya baba yao.
EmoticonEmoticon