Donald Trump Amsamehe Mshauri Michael Flynn

 

Rais Donald Trump amemsamehe mshauri wa zamani wa usalama wa taifa Michael Flynn, akilenga moja kwa moja katika siku za mwisho za utawala wake katika uchunguzi wa Russia ambao kwa muda mrefu amesisitiza ulitokana na upendeleo wa kisiasa. 

Trump alitangaza msamaha huo Jumatano, na kuuita Heshima Kuu.

Flynn ni mshirika wa pili wa Trump aliyehukumiwa katika uchunguzi wa Russia kupewa msamaha na rais. Trump alibadilisha adhabu ya rafiki wa muda mrefu Roger Stone siku chache kabla ya kwenda gerezani. 

Ni sehemu ya juhudi pana ya kutengua matokeo ya uchunguzi ambao uligubika utawala wake na kutoa mashtaka ya jinai dhidi ya nusu ya washirika wake.


EmoticonEmoticon