Donald Trump Baada Ya Matokeo Ya Uchaguzi Ni Mwendo Wa Golf

 

Katika kipindi cha miaka minne iliopita , nimemuona rais Donald Trump katika siku nzuri na katika siku mbaya. 

Lakini tarehe 7 mwezi Novemba , siku ambayo alipoteza uchaguzi ilikuwa siku tofauti kabisa.

Akiwa amevalia suruali nyeusi ,na kofia nyeupe ilioandikwa Make America Great Again MAGA , rais aliondoka katika ikulu ya whitehouse dakika chache kabla ya saa nne.

Alikuwa amuhudumia kipindi kirefu cha siku yake akituma jumbe zwa twitter kuhusu udanganyifu aliodai kufanyika katika uchaguzi.

Aliingia katika gari jeusi na kuelekea katika klabu yake ya kucheza gofu , Trump National Sterling , iliopo huko Virginia takriban kilomita 40 kutoka Ikulu ya Whitehouse .

Wakati huo alionesha matumaini . Ilikuwa siku nzuri kwa kucheza gofu na alikuwa anaenda kuhudumia siku hiyo katika klabu hiyo.

Lakini watu waliokwa wakimfanyia kazi waliathiriwa na matokeo hayo.

'Je unaendelejae', nilimuuliza mmoja ya wafanyakazi wake . 'Nashukuru'. alijibu . Alitabasamu. Lakini macho yake yakatazama simu yake.


EmoticonEmoticon