Ethiopia Yakataa Mkono Wa Maridhiano Wa AU Katika Mzozo Wa Tigray

 

Serikali ya Ethiopia imekataa juhudi za Umoja wa Afrika za upatanisho na kusema wanajeshi wake wamechukua udhibiti wa mji mwengine wakati jeshi la serikali linapoelekea katika mji mkuu wa mkoa wa kaskazini wa Tigray unaoshikiliwa na waasi. 

Mnamo siku ya Ijumaa, Umoja wa Afrika uliwateua marais wa zamani wa Msumbiji Joaquim Chissano, Ellen Johnsof Sirleaf wa Liberia na Kgalema Motlanthe wa Afrika Kusini kama wajumbe maalum katika mazungumzo ya upatanisho.

Zaidi ya wiki mbili baada ya Waziri Mkuu Abiy Ahmed kutangaza oparesheni ya kijeshi, serikali imesema vikosi vya usalama vya Tigray vinaharibu barabara na madaraja ili kuudhibiti mji mkuu wa mkoa wa Tigray, Mekelle, wenye idadi ya kiasi ya watu nusu milioni.

Wapiganaji wa Tigray wameahidi kupambana vikali na maadui zao. Hata hivyo, wamekanusha madai kuwa wameharibu madaraja na barabara.Mamia ya watu wamekufa na zaidi ya wengine 30,000 wamekimbilia Sudan tangu mzozo huo ulipoanza Novemba 4.


EmoticonEmoticon