Jumuiya ya Ulaya (EU) imetoa wito
kwa Serikali ya Marekani kusitisha utekelezaji wa hukumu ya kifo ya unyongaji
iliyoanzishwa tena kufuatia uamuzi uliochukuliwa.
Peter Stano
ambaye ni Msemaji wa Kamati ya EU, alitoa maelezo kuhusu suala hilo na
kubainisha hofu waliyokuwa nayo dhidi ya Serikali ya Marekani kwa kuanza tena kutekeleza
hukumu ya kifo ya unyongaji kufuatia uamuzi uliochukuliwa baada ya takriban
miaka 20.
Akisisitiza
kuwa EU inapinga vikali hukumu ya kifo, Stano alisema kwamba unyongaji ni
hukumu ya kikatili inayokiuka haki za kibinadamu, na haiwezi kusawazisha makosa
ya mtuhumiwa baada ya utekelezaji.
“EU inatoa wito kwa serikali ya
Marekani kuondoa uamuzi huo na kusitisha hukumu zote za kifo za unyongaji
zilizotolewa na ngazi za juu.” Stano
Stano pia
alifahamisha kuwa hukumu nyingi za kifo zilizotekelezwa na serikali ya Marekani
ya ngazi za juu zinatofautiana na hukumu za serikali za majimbo na dunia nzima
kwa ujumla.
Baada ya uamuzi kuhusu hukumu ya kifo kuchukuliwa tena mwezi Julai, serikali ya Marekani ilitekeleza hukumu hiyo na watu 8 wakanyongwa.
EmoticonEmoticon