Habari Tano Kubwa Za Soka Jumapili November 08

Tetesi Za Soka Ulaya Jumapili November 8, 2020

1. David Beckham anataka mchezaji wa zamani wa Real Madrid Sergio Ramos kuichezea Inter Miami wakati kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 itakapokamilika msimu ujao.

2. West Ham United inatarajiwa kuwasilisha ombi la £30m kumnunua mshambuliaji wa Lyon na Ufaransa Moussa Dembele iwapo klabu hiyo ya ligue 1 itaamua kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24.

3. Meneja mkuu wa klabu ya Lyon Vincent Ponsot amefichua kwamba Arsenal ni miongoni mwa klabu tatu mbazo zilikuwa zinamnyatia kiungo wa kati wa Ufaransa Houssem Aouar katika dirisha la uhamisho lililopita lakini ilitoa dau la chini ya thani ya mchezaji huyo mwenye umri wa kiaka 22.

4. Mshambuliaji wa Tottenham Hotspur na England Harry Kane, 27, anaamini Spurs ina fursa nzuri ya kushinda ligi ya Premia msimu huu.

5. Kiungo mshambuliaji wa Manchester City na England Phil Foden , 20 anatarajiwa kupatiwa mkataba mpya ambao utaongeza mara tatu mshahara anaopata kwa sasa.


EmoticonEmoticon