Habari Tano Kubwa Za Soka Jumatano November 11

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano November 11, 2020

1. Klabu ya Paris St-Germain itafirikiria kuwasilisha ombi la kumsajili winga wa Juventus Cristiano Ronaldo iwapo klabu hiyo ya Itali itaamua kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35. 

2. PSG pia imeanza mazungumzo ya kumpatia kandarasi mpya mshambuliaji wa Brazil Neymar, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 akifurahia kutia saini kandarasi mpya ya miaka mitano.

3. Aliyekuwa beki wa Liverpool Jamie Caragher anaamini kwamba Man United inafaa kumuuza kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba 27.

4. Arsenal ni miongoni mwa baadhi ya klabu ambazo zinamuwania mshambuliaji wa Sao Paulo na Brazil Brenner, 20.

5. The Gunners pia wameanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Red Bull Salzburg Dominik Szoboszlai, 20. Arsenal inafikiria kuwasilisha ombi la £22m kumnunua mchezaji huyo wa Hungary. 


EmoticonEmoticon