Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa November 6

 

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa November 6, 2020

1. Manchester United imezungumza na kocha wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino kuhusu kuchukua nafasi ya Ole Gunnar Solskjaer. Nafasi ya Solskjaer iko katika hatihati baada ya vipigo vya mfululizo na anaweza kufukuzwa ikiwa United itapoteza kwa Everton siku ya Jumamosi. 

2. Klabu kubwa za Ulaya zikiwemo Manchester City, Barcelona na Juventus, zinamfuatilia washambuliaji wa Borussia Monchengladbach Marcus Thuram,23 na Alassane Plea,27.

3. Real Madrid huenda wakamsajili kiungo wa kati, Mfaransa Paul Pogba,27, kutoka Manchester United kwa kitita cha pauni milioni 54 msimu ujao.

4. Klabu ya Bundesliga, Schalke inaweza kuridhia kumruhusu beki wa kati Mturuki Ozan Kabak,20 , kuondoka kwa pauni milioni 18 mwezi Januari. Hata hivyo mabingwa wa England, Liverpool wanamuhitaji mchezaji mwenzake, Mfini, Malick Thiaw, 19.

5. Arsenal wanajiandaa kujadili kuhusu kuongeza mkataba wa kiungo wa kati wa Misri Mohamed Elneny,28, aliyewavutia tangu mwanzo wa msimu. 


EmoticonEmoticon