Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa November 13

 

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa November 13, 2020

1. Manchester United wamewasilisha rasmi dau la kumnunua Cristiano Ronaldo kwa ajenti wake katika jaribio la kumsajili mshambuliaji huyo wa Portugal kutoka Juventus. Mabingwa hao wa Serie A wako tayari kumuachilia nyota huyo wa miaka 35 wasiposhinda Champions League.  

2. Arsenal, Chelsea na Tottenham zinamtaka beki wa Bayern Munich Jerome Boateng. Mjerumani huyo aliye na umri wa miaka, 32, huenda akaondoka kwa uhamisho wa bila malipo baada ya Bayern kuonesha ishara kwamba haina mpango wa kumpatia mkataba mpya. 

3. Chelsea inatarajiwa kuwasilisha dau lingine la kumnunua kiungo wa kati wa West Ham na England Declan Rice mwezi Januari. The Blues watawauza wachezaji wawili wakubwa kufadhili uhamisho wa Declan Rise aliye na miaka 28.

4. Liverpool wanatafakari uwezekano wa kumnunua mlinzi wa zamani wa Uholanzi na Watford Daryl Janmaat, 31, kama hatua ya muda mfupi ya kuimarisha safu yake ya ulinzi inayokabiliwa na changamoto. 

5. Real Madrid inatarajiwa kuwapunguzia tena marupurupu wachezaji wake kutokana na athari za janga la virus vya corona. 


EmoticonEmoticon