Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Ijumaa November 20

 

Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa November 20, 2020

1. Manchester City wameazimia kusaini mkataba na mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 33, baada ya meneja Pep Guardiola kukubali mkataba mpya.

2. Manchester United watapambana na Paris St-Germain na Real Madrid katika kumsaini kiungo wa kati Mfaransa mwenye umri wa miaka 18 kutoka klabu ya Rennes Eduardo Camavinga. 

3. Mshambuliaji Olivier Giroud, 34, yuko tayari kuangalia uwezekano wa ofa ya kuondoka Chelsea mwezi Januari kwa lengo la kuendelea mchezo wake katika kikosi cha Ufaransa kwa ajili ya msimu ujao wa kombe la Ulaya. 

4. Klabu kadhaa za Ligi ya Primia zinataka kumsaini beki wa uhispania Sergio Ramos, iwapo kijana huyo mwenye umri wa miaka 34 hataongeza mkataba wake Real Madrid .

5. Everton wanaangalia uwezekano wa kumsaini winga Manchester United na Wales Daniel James, 23, mwezi January.


EmoticonEmoticon