Tetesi Za Soka Ulaya Ijumaa November 27, 2020
1. Barcelona huenda ikamnyatia
mshambuliaji wa Liverpool raia wa Senegal Sadio Mane, 28, au kiungo wa kati wa
Uholanzi Gini Wijnaldum, 30, baada ya kipengee katika makubaliano yaliyowezesha
Philippe Coutinho kwenda Nou Camp kumalizika - Barca kusajili mchezaji mwingine
wa Liverpool italazimika kulipa kitita cha ziada cha pauni milioni 89.
2. Manchester United bado
haijakata tamaa ya kumsajili mchezaji wa Barcelona Ousmane Dembele lakini
itajitahidi kufikia makubaliano ya mkopo kwa mshambuliaji huyo wa Ufaransa, 23.
3. Manchester United imetoa ofa
mpya kwa mchezaji Timothy Fosu-Mensah,22, wa Uholanzi anayeweza kucheza nafasi
kadhaa ambaye mkataba wake unamalizika msimu ujao.
4. Mgombea urais wa Barcelona
Emili Rousaud anasema ikiwa atachaguliwa atasajili "wachezaji wawili
wazuri, mmoja wao akiwa Neymar", mshambuliaji wa Brazil, 28, ambaye
aliweka rekodi ya dunia ya uhamisho kutoka Barca hadi Paris St Germain mwaka
2017.
5. Lyon imetupilia mbali hatua ya kumsaka mchezaji wa Arsenal Houssem Aouar kwasababu ya mchezo wa Jumapili dhidi ya Reims ambapo kiungo huyo wa kati, 22, raia wa Ufarasa alikataa kupasha misuli moto kwasababu hakutumika kama mchezaji wa akiba kwenye mechi hiyo dhidi ya Angers walioibuka na ushindi.
EmoticonEmoticon