Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne November 3

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne November 3, 2020

1. Manchester City inaweza kumpa ofa mshambuliaji wa Barcelona na Argentina Lionel Messi, 33, ya mkataba wa awali mwezi Januari kabla ya kuhamia England msimu ujao.

2. Manchester City wanajiandaa kumfanya mshambuliaji wa England Raheem Sterling, 25 na kiungo wa kati wa Kibelgiji Kevin de Bruyne,29 kuwa wachezaji wanaolipwa pesa nyingi zaidi katika ligi ya Primia.

3. Paris St-Germain itakuwa makini katika uhamisho wa mchezaji wa England anayekipiga Tottenham Dele Alli,24, ikiwa atapatikana mwezi Januari. Klabu hiyo ya ufaransa ilifanya majaribio matatu yaliyogonga mwamba ya kumsajili kwa mkopo kiungo huyo wa kati msimu huu.

4. Barcelona imeongeza nia yake ya kumnasa mshambuliaji wa Benfica na Uruguay Darwin Nunez,21, kama mbadala wa muda mrefu wa Luis Suarez.

5. Atletico Madrid imeingia katika ushindani na Bayern Munich na Sevilla zikimfuatilia kwa karibu beki wa kulia wa Brighton Tariq Lamptey, 20. 


EmoticonEmoticon