Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumanne November 24

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumanne November 24, 2020

1. Pep Guardiola anataka Manchester City kumsajili Jack Grealish, baada ya kubaini kiungo huyo wa kati wa Aston Villa na England, 25, kama kipaumbele chake katika mipango yake ya kuunda kikosi kipya.

2. Kocha wa Man United Ole Gunnar Solskjaer anasisitiza mlinda lango Dean Henderson "anataka kusalia Manchester United", licha ya ripoti kuwa mchezaji huyo wa kimataifa, 23.

3. Kocha wa Chelsea Frank Lampard anasema mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 34, ambaye anataka kuhama kwingineko kutafuta fursa ya kuingia kwenye kikosi cha kwanza kabla Ligi ya Ulaya kuanza mwaka ujao, ni "mchezaji muhimu" na amesisitiza anataka asalie Stamford Bridge.

4. Borussia Dortmund iko tayari kuanzisha tena mikakati ya kumsaka kiungo wa kati wa Inter Milan raia wa Denmark Christian Eriksen, baada ya kuhusishwa na mchezaji huyo, 28, aliyekuwa Tottenham mapema mwaka huu.

5. Wakati huohuo Ole Gunnar Solskjaer amemuambia mshambuliaji wa Ufaransa Anthony Martial, 24, hawezi kutulia na tajiba yake yote akiwa Manchester United baada ya mwanzo mgumu wa msimu kwa timu hiyo.


EmoticonEmoticon