Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu November 16

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu November 16, 2020

1. Kiungo wa kati wa Manchester United na Ufaransa Paul Pogba anasema kwa sasa anapitia kipindi kigumu sana cha kazi yake ya soka kutokana na muda wake wa mchezo katika Old Trafford. 

2. Manchester City wanasaini mkataba na mshambuliaji ambaye ni kipaumbee chao cha mwaka 2021, nyota wa Borussia Dortmund Mnorway Erling Haaland, 20, na kiungo wa mbele wa Inter Milan Muargentina Lautaro Martinez, 23, ambao ndiye wachezaji wanaowalenga zaidi .

 3. Kiungo wa kati wa AC Milan Mturuki Hakan Calhanoglu, 26, huenda yuko njiani kuelekea Atletico Madrid baada ya mazungumzo ya mkataba na klabu hiyo ya Italia kukumbwana tatizo, ingawa Manchester United bado wanamtaka .

4. Juventus wako tayari kumnunua nyota mchanga anayechezea Ajax Ryan Gravenberch lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Barcelona katika kumsaini kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 18 tu .

5. Mchezaji wa safu ya ulinzi ya Chelsea Mjerumani Antonio Rudiger, 27,yuko makini kuhusu kujiunga na klabu ya Barcelona wakati dirisha la uhamisho litakapofunguliwa mwezi Januari baada ya kutopendelewa katika Stamford Bridge.


EmoticonEmoticon