Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatano November 18

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano November 18, 2020

1. Mshambuliaji wa zamani wa Manchester City na Liverpool Mario Balotelli amefanya mazungumzo na timu ya Championi ya Barnsley. Muitalia huyo mwenye umri wa miaka 30 , yuko huru baada ya mkataba wake na Bresica kusitishwa kwa kutohudhuria mazoezi .

2. Leicester wanamfuatilia kwa karibu kiungo wa safu ya nyuma -kushoto Mreno Nuno Mendes, 18, ambaye anakipengele cha kumnunua cha pauni milioni 40 katika mkataba wake na Sporting Lisbon.

3. Meneja Pep Guardiola bado hajaamua kuhusu hali yake ya baadaye katika Manchester City. Mkataba wake unaisha msimu huu.

4. Chelsea wanataka kusaini mkataba na kiungo wa Borussia Dortmund na England Jude Bellingham, mwenye umri wa miaka 17 badala ya kiungo wa kati wa West Ham Declan Rice, 21.

5. United watapatia kipaumbele mauzo ya wachezaji mwezi wa Januari huku mlinzi wa England Phil Jones, 28, na Waagerntina mlinda lango Sergio Romero, 33, na beki Marcos Rojo,30, wakiwa na uwezekano mkubwa wa kuondoka katika klabu hiyo.


EmoticonEmoticon