Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Alhamisi November 19

 

Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi November 19, 2020

1. Lionel Messi amewatahadharisha Manchester City kabla ya dirisha la uhamisho wa wachezaji la uhamisho baada ya mshambuliaji huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 33, kusema kuwa "amechoka kuwa kila siku kuwa yeye ndio tatizo " katika Barcelona.

2. Real Madrid wanakabiliana na Barcelona katika kinyang'anyiro cha kumsaini kiungo wa kati Mholanzi Georginio Wijnaldum, 30, kutoka Liverpool. 

3. Liverpool na Manchester United wamepata hamasa ya kumnunua mchezaji wa RB Leipzig Dayot Upamecano kutokana na uamuzi wa kiungo huyo wa safu ya nyuma-kushoto kuhusu hali yake ya siku za usoni utachukuliwa Januari na Bayern Munich imekwisha ashiria kuwa haina uwezo wa kumsaini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22.

4. Mlinzi wa Bayern Munich na Austria David Alaba, 28 ndiye mchezaji anayelengwa zaidi na Real Madrid kama kiungo wa kati-nyuma wa Uhispania Sergio Ramos ataondoka katika klabu hiyo msimu huu .

5. Manchester United h wana fursa ya kusaini mkataba na kiungo wa kati- Mfaransa Raphael Varane, 27, kutoka Real Madrid. 


EmoticonEmoticon