Habari Tano Kubwa Za Soka Ulaya Jumatatu November 23

 

Tetesi Za Soka Ulaya Jumatatu November 23, 2020

1. Manchester City imesitisha harakati zake za kutaka kumsajili mshambuliaji nyota wa Barcelona Lionel Messi, 33, kulingana na mtaalamu wa soka wa Uhispania Semra Hunter.

2. Arsenal imepigwa jeki katika harakati zake za kumsajili kiungo wa kati wa Uturuki Yusuf Yazici baada ya ajenti wake kukiri kwamba mchezaji huyo huenda akaondoka katika klabu ya Lille. Mchezaji huyo amefananishwa na kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil 32. 

3. Kipa wa klabu ya Manchester United Dean Henderson, 23, atafuatilia uhamisho wake wa mkopo ili kuimarisha hadhi yake katika kushiriki kombe la mabingwa Ulaya huku klabu za Leeds na Brightong zikihusishwa na ununuzi wa mchezaji huyo mwezi Januari.

4. Aliyekuwa kiungo wa kati wa Tottenham Christian Eriksen, 28, yuko huru kuondoka Inter Milan mwezi Januari , afisa mkuu wa klabu hiyo ya Itali Beppe Marotta amethibitisha.

5. Jeraha la mguu la beki wa Barcelona na Uhispania Gerard Pique, 33, huenda likabadilisha jinsi klabu hiyo itakavyomtafuta beki mwengine mwezi Januari kujaza pengo lake. Mabingwa hao wa Catalan wana hamu ya kumsajili beki wa Manchester City na Uhispania Eric Garcia, 19. 


EmoticonEmoticon