Tetesi Za Soka Ulaya Jumatano November 25, 2020
1. Real Madrid imejibu tetesi za
Raphael Varane kuhusishwa na Manchester United kwa kusema mlinzi huyo wa
Ufaransa, 27, "hawezi kuuzwa".
2. Arsenal iko tayari kufanya
mazungumzo na Nicolas Pepe baada ya kupewa kadi nyekundu huko Leeds Jumapili
lakini hakuna uwezekano wa kufikiwa kwa makubaliano ya mkopo dhidi ya
mshambuliaji huyo wa Ivory Coast forward, 25, Januari.
3. The Gunners pia inamwinda
kiungo wa kati wa Sheffield United Sander Berge licha ya kumkosa raia huyo wa
Norway, 22, Januari iliyopita alipohamia Bramall Lane.
4. Arsenal inamfuatilia aliyekuwa
mchezaji wao Yunus Musah, 17, huku Everton, Leeds na Wolves zikiwa zimeonesha
nia ya kutaka kumsajili winga huyo wa Valencia, ambaye pia ni mchezaji wa
kimataifa Marekani.
5. Chelsea tayari inafanya mazungumzo na mlinzi wa Brazil Thiago Silva, 36, kuhusu kuongezwa kwa kandarasi yake kwa mwaka mwingine hadi 2022.
EmoticonEmoticon