Tetesi Za Soka Ulaya Alhamisi November 26, 2020
1. Arsenal wamepatiwa fursa ya
kumsaini kiungo wa kati wa Inter Milan Christian Eriksen katika makubaliano ya
bei ya chini miezi 10 baada ya raia huyo wa Denmark , 28, kuondoka Tottenham.
2. Everton inawachunguza wachezaji
watatu wa Tottenham kabla ya dirisha la uhamisho la mwezi Januari - kipa Paulo
Gazzaniga, 28, Kiungo wa kati Delle Ali na Harry Winks wote wakiwa na umri wa miaka
24.
3. Kiungo wa kati wa West Ham
United na England Declan Rice, 21, anasema kwamba ni muhimu kushinda mataji
licha ya uvumi kuhusu ombi la kutaka kumsajili kutoka Chelsea mwezi Januari.
4. Inter Milan itajaribu kumsaini
mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud , 34 kutoka Chelsea mwezi Januari.
5. Beki wa Ufaransa William Saliba, 19, yuko tayari kuwacha mshahara wa £90,000 kwa wiki ili kupata uhamisho wa mkopo kutoka Arsenal mwezi Januari.
EmoticonEmoticon