Chanjo Inayoweza Kuzuia Corona Kwa 90% Imepatikana

 

Chanjo ya kwanza ya virusi vya corona ambayo inaweza kuzuia zaidi ya asilimia 90 ya watu kupata Covid-19, utafiti wa awali umebaini.

Wavumbuzi - Pfizer na BioNTech -wanaelezea kuwa ni siku nzuri kwa wanasayansi na kila mtu.

Chanjo yao imewafanyia majaribio watu 43,500 kutoka nchi sita na hakuna wasiwasi wa usalama wao ulioibuka.

Makampuni yamepanga kuomba ruhusa ya dharura ya kutumia chanjo hiyo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu.

Chanjo hiyo inaonekana kuwa tiba nzuri, na inaonekana kuwa njia sahihi ya kukabiliana na marufuku zilizowekwa dhidi ya corona na maisha kurejea kuwa kama kawaida.

Kuna hatua kadhaa za kumaliza jaribio hilo - hatua inayojulikana kuwa jaribio la tatu - lakini jaribio hili ni la kwanza kuonyesha matokeo ya namna hiyo.

Jaribio hili limetumia sindano na vina vya virusi ili kuuweka sawa mfumo wa kinga .

Majaribio ya awali yanaonesha kuwa chanjo inaweza kuweka sawa kinga za mwili -na mfumo mwingine wa kinga ya seli katika kukabiliana na virusi vya corona.

Dozi mbili, ndani ya wiki tatu ndio inahitajika.

Majaribio hayo yamefanyika Marekani, Ujerumani, Brazil, Argentina, Afrika Kusini na Uturuki -yanaonesha kuwa ina kinga kwa 90% ndani ya siku saba baada ya kupata dozi ya pili.

Pfizer inaamini kuwa inaweza kutoa dozi milioni 50 mwishoni mwa mwaka huu, na bilioni 1.3 mwishoni mwa mwaka 2021.

Ingawa kuna changamoto za kitakwimu , kwa kuwa chanjo hiyo inahitajika kuhifadhiwa kwa kiwango cha ubaridi wa 80C.


EmoticonEmoticon