Instagram Waombwa Kufanya Uchunguzi Papa Aliipenda Vipi Picha Ya Mlimbwende

 

Vatican imewaomba Wamiliki wa Mtandao wa kijamii wa Instagram kuchunguza ni namna gani akaunti ya Papa Francis imeweza ku-like picha ya nusu uchi ya Model Natalia Garibotto.

Msemaji wa Vatican amesema LIKE hiyo haioneshi kuwa imetokea kwa Watu wanaoendesha akaunti ya Papa Vatican na huenda akaunti imedukuliwa "bado tunachungua pia kama kuna Mtu kati ya wanaondesha akaunti amehusika ku-like tutajua"

Natalia na Kampuni inayomsimamia wameendelea kukoleza moto kwa kutumia like ya Papa kujiongezea umaarufu ambapo Natalia ameandika kwenye Twittter kuwa "At least naenda Mbinguni, kama Papa Francis amekubali kazi, wewe ni nani? safari ya Vatican imeiva"


EmoticonEmoticon