Iran: Tutaheshimu Mkataba Wa Nyuklia Endapo Biden Ataondoa Vikwazo

 

Iran imesema itaanza kuheshimu majukumu yake katika mkataba wa nyuklia, endapo rais mteule wa Marekani Joe Biden ataondoa vikwazo vilivyowekwa miaka miwili iliyopita. 

Waziri wa mambo ya kigeni wa Iran Mohammad Javad Zarif, amesema Tehran inaweza kurejea katika kuheshimu majukumu yake bila ya kuwepo na masharti au hata mazungumzo. 

Mivutano ya muda mrefu baina ya Iran na Marekani iliongezeka baada ya rais Donald Trump, kujiondoa kutoka makubaliano ya nyuklia mnamo mwaka 2018 na kuanzisha tena vikwazo vikali. 

Wakati Trump akitaka kuongeza shinikizo dhidi ya Iran na kuitenga na ulimwengu, Biden ameashiria kulipatia taifa hilo la Kiislamu njia ya kuaminika ya kurudi kwa diplomasia. 

Zarif amedai Marekani inawajibika kutekeleza azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilifikia makubaliano ya mwaka 2015.


EmoticonEmoticon