Katika
maeneo ya biashara Ulaya ambako watu kwa kawaida hukusanyika katika vibanda
ambavyo vimefurika watu kupata viburudisho vya mvinyo moto, mkate wa tangawizi,
sausage na vyakula vya tunu vingine hivi sasa ni viwanja vitupu.
Masoko ya Krismasi, utamaduni unaoenziwa nchini Ujerumani na
nchi jirani, yamejiunga katika orodha ndefu ya utamaduni wa kila mwaka ambao
umefutwa au umepungua mwaka huu kwa sababu ya janga la virusi vya corona,
Shirika la habari la AP linaripoti.
Mwezi Novemba ulishuhudia nchi nyingi za Ulaya zikiweka
baadhi ya masharti au katazo kali la kutotoka nje wakati maambukizi mapya ya
virusi yakiongezeka.
Masharti hayo ama yanaendelezwa au baadhi yamelegezwa wakati
wa kusubiriwa kwa mazao ya Yesu maarufu kama Advent ikianza Jumapili.
Moja ya masoko ya sikukuu yaliyo bora na ya kiasili ni sehemu
inayowaleta watalii wengi, yalitangazwa kutofunguliwa mwezi mmoja uliopita.
Masoko nchini kote --- ikiwemo Frankfurt, Dortmund na Berlin
--- yameathiriwa na hali hiyo pia, ambapo mamlaka zimesitisha shughuli
mbalimbali au waandaaji wakiamua kuwa haiingii akilini kulazimisha mipango yao
iendelee.
Kwenye mpaka wa Ufaransa, takriban vibanda 300 vya biashara maarufu ya Krismasi huko Strasbourg havitafunguliwa mwaka huu. Na ni hali hiyo hiyo katika mji mkuu wa Ubelgiji, Brussels.
EmoticonEmoticon