Jimbo La Georgia Marekani Kuhesabu Kura Upya Kwa Mikono Na Sio Mashine

 

Ofisa wa Uchaguzi katika Jimbo la Georgia Nchini Marekani Brad Raffensperger jana ametangaza kuwa, Jimbo hilo litarudia kuhesabu upya kura za Uchaguzi wa Urais>> "kura zitahesabiwa kwa mkono bila mashine ili kuondoa utata, ni zoezi gumu ila tutapambana hadi Nov 20 tukamilishe"

Kwa mujibu wa NBC, Joe Biden ameongoza dhidi ya Rais Donald Trump kwa zaidi ya kura 14,000 kati ya kura Milioni 5 zilizopigwa kwenye Jimbo hilo, pia Brad ameiambia CNN kuwa wameamua kurudia tena kwa kutumia mkono na sio mashine ili kuondoa malalamiko yaliyopo.

Donald Trump bado ameendelea kutokubaliana na ushindi wa Joe Biden na ameendelea kuomba kurudiwa kwa kura katika Majimbo karibu yote huku akipambana pia kutafuta msada wa kisheria Mahakamani kupinga matokeo hayo ambayo anasema yametawaliwa na wizi wa kura.


EmoticonEmoticon